April 17 2018 2Comments

WANANCHI 20,000 KUONDOKANA NA ADHA YA MAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA

Wananchi zaidi ya 20,000 wa Vijiji vya Magombwe,Isele,Kinyika na Kisanga wataondokana na adha ya maji mara baada ya Miradi miwili ya upanuzi wa Mradi wa maji Pawaga kwenda vijiji vinne Kata ya Mlenge kukamilika.
Akiongea wakati wa hafla ya utiaji sahihi wa Mikataba miwili ya Upanuzi wa Mradi wa maji Pawaga kwenda Vijiji vine vya Kata ya Mlenge, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bw.Robert Masunya amewataka Wakandarasi waliochaguliwa kutekeleza Miradi hii miwili ya maji kufanya kazi kwa uadilifu na kuachana na masuala mengine ambayo yatakwamisha kutekeleza Miradi hii kwa wakati huku akiwakumbusha kuwa wanalo jukumu kubwa kuhakikisha kuwa Miradi inayotekelezwa inajengwa kwa ubora unaoelezwa katika mikataba iliyosainiwa.
Pia amewataka kukamilisha Miradi hii katika muda wa mkataba ili uanze kutoa huduma kwa wananchi mapema ili kuleta maendeleo yanayohitajika na wananchi.
Aidha ameonya suala la rushwa lisiingizwe katika kazi, ‘’Mimi siamini kama tunaishi kwa rushwa,nimesimamia Miradi mikubwa ya maji ukerewe bilioni 13, Miradi ya Sengerema bilioni 21, kwa hiyo siyo kwamba hiyo bilioni 4 kwangu itanipa shida naona ni kitu cha kawaida tu,na haitaniondolea uimara wangu,mimi nitasimamia Miradi hii kwa uimara na kuhakikisha inatoa matokeo makubwa’’. Alisema Bw. Masunya.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mhe.Steven Mhapa amewataka Wakandarasi waliochaguliwa kutekeleza Miradi hii kufanya kazi kwa ufanisi na uaminifu mkubwa na kampuni itakayoshindwa kufanya kazi katika ubora unaotakiwa hatasita kutoiruhusu kufanya kazi ndani ya Halmashauri yake.
Mh.Mhapa pia amewataka wakandarasi washirikiane na wananchi katika ngazi za kata na vijiji ili kuhakikisha ushiriki wa wananchi katika Miradi inayowazunguka.
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa imesaini Mikataba miwili ya upanuzi wa Mradi wa maji yenye thamani ya shilingi bilioni 4.8,Mikataba hiyo ni Upanuzi wa Mradi wa maji Pawaga kwenda vijiji vine vya kata ya Mlenge,kujenga mabomba ya kusambaza maji kwenda Magombwe, Isele, Kinyika na Kisanga chini ya Mkandarasi GNMS Contractors LTD wa S.L.P 107 Iringa kazi hii itagharimu shilingi bilioni 3,216,845,931 na itatekelezwa kwa muda wa miezi 18.
Na Mkataba wa pili ni Upanuzi wa Mradi wa Maji pawaga kwenda vijiji vine vya Kata ya Mlenge,Ujenzi njia kuu mpya ya usambazaji 14.6km kutoka tanki la maji masafi kwenda kwenye tanki la luganga na Magozi, kutengeneza kituo cha kusafishia maji,tanki Ilolompya 50m3, Kimande 75m3 na Mbuyuni chini ya Mkandarasi M/S HEMATEC INVESTMENT LTDwa S.L.P 34078 Dar-es-salaaam,kazi hii itagharimu shilingi bilioni 1,647,262,810 na itatekelezwa kwa muda wa miezi 12.

admin

2 comments

  1. Wishing you good luck in implementing project (Construction)

    Reply
    1. thanks Jackson moris

      Reply

Write a Reply or Comment